Masaibu ya Mackenzie yazidi, apatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwanyima chakula
Fri, 27 Nov 2026 14:50:25 +0000
Kiongozi wa dhehebu la Good News International, Paul Mackenzie, amepatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwashawishi kufunga hadi kufa katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.
Hata hivyo, Mahakama Kuu ilimwachilia huru katika mashtaka mengine 115 yaliyohusisha vifo vya waathiriwa wengine, ikisema upande wa mashtaka haukuthibitisha chanzo cha vifo hivyo bila shaka yoyote.
Jaji Alex Ithuku alisema Mackenzie ndiye aliyepanga mpango wa kufunga, akatoa maagizo kuhusu nani angekufa kwanza na kue...
Obado kula maharagwe jela miaka 25 kwa mauaji ya Sharon Otieno
Fri, 27 Nov 2026 09:19:13 +0000
Aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno na mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa mwaka 2018.
Mahakama Kuu ya Milimani pia ilimhukumu aliyekuwa msaidizi wake wa kibinafsi Michael Juma Oyamo kifungo cha miaka 25, huku aliyekuwa mfanyakazi wa serikali ya kaunti ya Migori Caspal Ojwang Obiero akifungwa miaka 18.
Hukumu hizo zilitolewa na Jaji Cecilia Githua jana.
Sharon alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili k...